Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu shirika la Anadolu, mmoja wa wasafiri wa msafara wa “Sumud”, huku akirejelea yaliyotokea katika njia ya safari ya msafara huo wa baharini, alisema kwamba; meli yao ilisimamishwa katikati ya safari na vikosi vya Israel. Kwa mujibu wake, abiria baada ya kukamatwa walihamishiwa kwenye meli nyingine ambayo ilionekana kuwa ilikuwa imeandaliwa mapema kwa ajili ya kuwashikilia.
Aliongeza kwamba; mazingira ya kushikiliwa yalikuwa magumu sana, na takribani watu 60 waliwekwa ndani ya makontena matatu madogo; kwa namna ambayo kila kontena lenye nafasi ndogo lilikuwa na karibu watu 20 ndani yake.
Msafiri huyo alisema; mmoja wa wenzao aliyeitwa “Saif” alitoweka baada ya kukamatwa, na abiria walikataa kuhamishwa tena hadi walipopata taarifa kuhusu hali yake, lakini baada ya malalamiko hayo walikabiliwa na ukatili mkubwa zaidi. Aliongeza kwamba; hata baadhi ya wanawake waliokuwemo katika msafara huo, wakiwemo madaktari, walipigwa.
Katika kuelezea vikosi vya Israel alisema: “Walikuwa na miili mikubwa sana, lakini walikuwa waoga.”
Aliongeza kwamba; baada ya siku kadhaa, abiria walihamishwa hadi kwenye kisiwa kilicho karibu na Greece, na baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu huko.
Msafiri huyo pia alizungumzia kupotea kwa mali zake binafsi na kusema kwamba kiasi cha euro elfu moja kilichukuliwa kutoka kwenye pochi yake, na licha ya kwamba vikosi vya Israel vilidai kuwa walivikabidhi kwa maafisa wa Ugiriki, maafisa wa Ugiriki hawakuthibitisha jambo hilo.
Maoni yako